Rumors zimezidi kusambaa kuhusu Samsung Galaxy S5 ambayo itatoka January mwakani. Tetesi mpya kabisa kuhusu simu hiyo inayosubiriwa na wengi ni kwamba S5 itakuwa na ‘kidude’ ambacho kitakuwezesha wewe kuseti scan ya macho kama njia ya kutoa password.
Kwa watumiaji wa Android wa sasa, kuna njia tatu kuu za kutoa loki ya simu ambazo ni password ya namba, kuchora pattern, na kuscan sura ambayo nimeiona kwenye Galaxy S2 – sina uhakika kama inapatikana kwenye matoleo mengine chini ya S2 au toleo lolote la simu zingine zenye android ukitoa Samsung.
Sasa, hii mpya italeta njia nyingine ya 4: Kuscan macho. Kama wewe ni mpenzi wa movies kama mimi basi utakuwa umeshawahi kuona hii kitu. Samsung wanaileta kwenye simu.
Hii ni kujibu mapigo ya Apple kwenye iPhone 5 ambapo wameweka fingerprint scanning. Samsung wameamua kuchukua hatua moja mbele na kuleta Eye Scanning ili kuonyesha kuwa wao ni bora kuliko Apple. I love this.