Internet ni mtandao muhimu katika maisha yetu sasa. Unaweza kufanya biashara, kuangalia matokeo, filamu, muziki na mambo mengi kutaja machache tu.Spidi ya jinsi mambo yanavyopakuliwa mtandaoni hutofautana baina ya watumiaji wa mtandao huu.. Kwa kweli internet yetu Afric a bado ipo nyuma kidogo, tunapata spidi ndogo ukilinganisha na mabara mengine yaliyoendelea. Lakini hiyo sio sababu kubwa nyuma ya spidi ndogo ya internet ambayo wengi wetu tumekuwa tukipata.
Leo,
tutaangalia mambo 10 unayoweza kufanya ili kuongeza spidi ya internet
yako, lakini kabla ya kuanza inabidi kujua spidi ya sasa ya internet
yako na kama iko sawa au la. Kuangalia spidi ya internet yako Bofya Hapa. Au tafuta kupitia search engine kama google neno, Speed Test. Nilifanya zaid ya mara tatu nikapata wastani wa 0.83mb/s kwa Modem ya Airtel.
#10. Update Browser na Computer yako.
Browser
iliyopitwa na wakati inaweza kuwa chanzo cha internet kupakua kurasa na
mafaili taratibu. Browser hizi huboreshwa mara kwa mara. Jaribu ku
update browser yako kila mara. Computer pia ambayo haiko updated ni
chanzo kikubwa kwa matatizo mbalimbali ya computer. Jaribu ku update
computer yako kila siku. Ili ku update kama unatuma windows, Bofya Control Panel, Kisha System and Security halafu chagua Windows Update. Unaweza
kucheck li computer iwe na update automatically. Hii ni muhimu sio tu
kwa ajili ya internet bali kwa matumizi bora ya computer yako. Pia
unaweza kubadili browser, watu wengi hutumia Mozilla Firefox sababu tu
wamewekewa, nakushauri u download Google Chrome Hapa.#10. Update Browser na Computer yako.
#9. Ongeza Bandwidth kwa 20%
Ingia kama Adminstrator kwenye computer yako.
>>Bofya Start,
>>kisha Andika gpedit.msc, panua (yaani bofya kile kimshale kidogo) itatokea menyu chini >>yake, panua tena Local Computer Policy,
>>panua Administrative Templates.
>>Panua tena Network Branch,
>>Sasa bofya QoS Packet Scheduler
>>Angalia upande wa kulia, kisha bofya Limit Reservable Bandwidth,
Ukishaibofya hiyo, itatokea menyu ndogo upande wa kushoto wake, Kisha juu kabisa,
Bofya Edit Policy Setting.
Utaona namba ya Bandwidth imeandikwa 20%, badili iwe 0%.
Usijali, haujapunguza bali umeongeza spidi ya internet kwa asilimia 20, ulipoandika 0.
Nakushauri baada ya kufanya hivyo Restart Computer yako kisha fungua tena Browser yako.
#8. Hamisha Router yako.
Sio watumiaj wote wanatumia Modem. Kama unatumia router jaribu kutafuta sehemu ambayo iko wazi kidogo. Sehemu ambayo unaweza kupokea mawimbi kwa wingi. Kwa mfano kama Router ipo juu ya meza jaribu kuweka juu ya kabati. Usiweke juu au karibu ya TV, Redio na Computer kwani ndo kabisa huharbu mawasiliano.
#7. Ondoa vifaa vya kielektroniki vyenye sumaku.
Kama unatumia, internet karbu na vifaa vingine vya kielektroniki na vyenye sumaku kama Redio, Smart TV na Smartphones sogeza mbali au zima kama hazitumiki. Hizi hushindana na Modem katka kupukea mawimbi ya mawasiliano na pia zile sumaku zina repel.
#6. Scan Computer yako, safisha pia na CCleaner.
Kama hauna ccleaner Bofya Hapa KuDOWNLOAD, Tumia Antivirus yako saa zote uwapo mtandaoni. Ondoa virusi kwa kutumia Antivirus yako na kisha safisha Registry na Cache za Internet kwa kutumia CCleaner.
#5. Fupisha au badilisha Waya.
Watumiaj wa internet moja kwa moja kutoka katika dish la satelite ndio hupata internet ya kasi zaidi. Lakini internet pia inaweza kuwa na kasi ndogo, hii husababishwa na matatizo kama kuwa na watu wengi sana wanaotumia mtandao huo kwa wakati mmoja, au pia tatizo linaweza kuwa cable ndefu. Cable kutoka katika Server au Router inaweza kuleta data polepole, jaribu kupunguza urefu wa cable hii.
#4. Kata Programu nyingine zinazotumia internet katika Computer yako
Programu kama Antivirus, Windows Update na baadhi ya magemu hutumia internet saa nyingine bila hata kukutaarifu au kupata ridhaa yako. Pia kama katika browser yako kuna vipengele vya tovuti nyingi hizi huendelea kupakua data kutoka mtandaoni na hivyo kuendelea kutumia internet saa zote, jaribu kuzuia kwa kubonyeza ESC kwenye keyboard kwa kipengele ambacho hautaki kiendelee ku load. Jinsi ya kuzuia programu katika computer zinazotumia internet, kama kweli umedhamiria nakushauri ufanye hii pia.
>> BOFYA START
>>kisha chagua All Programs
>> Kisha chagua Accessories
>> Shuka chini kidogo halafu bofya folder la System Tools
>> Katika Menyu inayotokea chagua Resource Monitor.
>> Katika Resource Monitor bofya kitufe cha Network.
>> Hapa zinaonekana programu zinazotumia internet, acha programu chache tu zitumie lakini zile ambazo sio za msingi zikate. Jinsi ya kukata. Right-Click program usiyotaka itumie internet kisha chagua End Process.
#3. Badili channel yako ya Wi-fi
Kama unatumia wireless katika sehemu fulani hasa katika sehemu zenye watumiaji wengi, kuna uwezekano kwamba wi-fi hiyo ina mzigo mkubwa. Hama na tumia channel nyingine. Download Software Hii itakuonesha ni channel gani zipo maeneo uliyopo na idadi ya watumiaji.
#2. Ondoa Toolbars katika browser yako.
Mara nying unapodownload na ku install software fulani zinaongeza toolbars kwenye browser zako. Uninstall toolbars hizo. Ingia katika My Control Panel kisha angalia jina la toolbar, ibonyeze halafu Unistall.
#1. Chomoa Modem-Chomeka Tena. Zima Computer-Washa Tena. Funga Browser-Fungua Tena.
Kama haupendi kutumia muda mrefu, fanya hivyo tu. Joto ni moja wapo wa maadui wakubwa wa Computer, ukitumia computer kwa muda mrefu sana jaribu kuizima kidogo kuipa nafasi ya kupoa. Unaweza pia kuchomoa modem na kisha kuchomeka upya. Pia kama browser yako ilikua imefunguliwa kwa muda mrefu, jaribu kuifunga na kisha kuifungua tena.
Ni matumaini yangu kuwa baada ya kufanya yote hayo au hata baadhi utaona mabadiliko katika kasi ya internet. Nakushauri sana ku update computer yako mara kwa mara. Computer iliyo updated hufanya kazi vizuri zaidi ya ile ambayo haija updatiwa