Tumezoea kuona Application za Facebook ambazo nyingi zimetengenezwa na wenzetu na tunazitumia lakini kwa hivi karibuni kasi ya kuona App za michezo zilizotengenezwa hapa nchini imeongezeka. Uzuri wa kuwa na App zilizotengenezwa Africa ni kuwa zinalenga maisha ya mtu wa kawaida tofauti na za wenzetu ambazo zimewalenga wale walioko nchi za magharibi ambao maisha yao ni tofauti na ya kwetu. Mfano wa App hii ni DUME Love Tree ambayo ipo katika ukurasa wa Facebook wa DUME Condoms ikiwa imetengenezwa na kampuni ya AIM Group.
Mara ya kwanza nilipoona picha kwenye ukurasa wa Facebook kukiwa na maandishi “Je, wewe yeye na wengine wangapi? Jibu aprili 15″ nilihisi labda itakuwa takwimu iliyotokana na utafiti fulani inayoelezea idadi ya wapenzi ambayo mtu amewahi kuwa nao, nilipoifungua siku yenyewe ilipofika nikakutana na kitu tofauti. Hii ni kama calculator inayokupimia idadi ya wapenzi ambao inawezekana umewahi kuwahi nao bila wewe kujua kutokana na idadi ya wale ambao mpenzi wako amewahi kutembea nao.
Inafanyaje Kazi?
Unapobofya link hii: https://www.aymzz.com/apps/dumelovetree/ unakutana na kitu hiki hapa chini:
Ukishaifungua unakuwa na uwezo wa kuchagua lugha, kama unapenda kutumia kiswahili unabofya upande wa juu kulia na kama unapenda kutumia kiingereza unabofya “enter” kuendelea. Mimi nilichagua Kiswahili kisha nikabofya “Anza” ili kuingia kwenye App na kisha itakuonyesha maelezo kuhusu ilivyo kama inavyoonekana hapa chini:
Baaada ya kubofya “Endelea” itakuleta kwenye sehemu unayotakiwa kuandika jina lako na umri ili kuthibitisha kuwa una miaka zaidi ya 18 kama masharti ya kushiri yanavyosema kama inavyoonekana hapa chini:
Hatua itakayofuatia ni kuchagua sura yako unayoipenda ambayo wametengeneza sura ambazo asilimia kubwa ya watu wanazako kama inavyoonekana.
Hatua itakayofuatia ni kuingia katika sehemu ya kuchagua maelezo yanayokuhusu. Swali la kwanza utakaloulizwa ni umewahi kuwa na wapenzi wangapi, swali la pili litakuwa kati ya hao wangapi mlitumia kondomu wakati wa kufanya tendo na swali la tatu litakuwa ni kama unafahamu majibu yao kuhusu vipimo vya UKIMWI kisha utatakiwa kwenda mbele.
Ukishamaliza kitakachofuatia App itakupigia hesabu ya wapenzi ambao unaweza kuwa umeshiriki nao ngono kutokana na wao kuwa wameshiriki ngono na wapenzi wako wa zamani. Hesabu yangu sitaki kuificha kama inavyoonekana hapa chini:
Well, nina 160 kama inavyoonekana katika hesabu ya jumla. Nilipanic kiaina nilivyoona hiyo idadi. Kinachofuata baada ya kujua idadi yako ya wapenzi ni ushauri wa kitaalamu unaopewa mfano mimi kutokana na idadi yangu ya wapenzi nimeambiwa “Kwa kuzingatia maelezo uliyoandika, na kutokana na namba ya wapenzi, uko kwenye hatari ya kuwa kwenye maambukizi ya magonjwa ya ngono. Unashauriwa kwenda na kupima magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana mapema iwezeanavyo”.