Featured

    Featured Posts

    www.nteltanzania.blogspot.com

    Social Icons

    This technologyzaleo blogsite is all about scientist,innovators,computer maintanance and networking and any related technology. For more knowledge you may visit this site to get any new version of technologies together with lessons for how you can handle your matters.feel at your home and you're welcome
Loading...

MFUMO WA TECHNOLOJIA YA TIBA YA MBALI "TELEMEDICINE" NCHINI TANZANIA..!! FURAHIA ULIMWENGU WA TECHNOLOGY SASA



Mama yako mzazi yu mgonjwa mahututi katika hospitali ya Wilaya ya Masasi. Madaktari wamelifahamu tatizo lake lakini hakuna vifaa wala wataalamu wa jinsi ya kumtibu. Anatakiwa ahamishiwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako kuna madaktari bingwa na vifaatiba vya uhakika. Hata hivyo safari ya kutoka Masasi hadi Dar Es Salaam, pengine yaweza... kupoteza uhai wake.
Lakini usihofu... Tanzania sasa imepata neema baada ya kuwepo kwa huduma ya Tiba kwa njia ya Teknolojia ya habari na mawasiliano, kwa kitaalamu ‘telemedicine’ 
Telemedicine ni utoaji wa huduma za afya au mbadilishano wa taarifa za kitiba kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano.
Mafanikio ya uvumbuzi huu yamesaidia  wataalamu wa afya kubaini na kutibu wagonjwa bila kuonana nao uso kwa uso.
Kwa kifupi, unaweza ukazungumza na daktari wako na kumweleza vile unavyojisikia, kisha akakuandikia vipimo, na baada ya kumpa majibu ya vipimo hayo kwa njia ya teknolojia pia, atakuandikia dawa au kukupa ushauri wa kitiba.
 Pia, Hospitali yenye vifaa na wataalamu wanaweza kuzungumza na madaktari katika hospitali za vijijini na kutoa ushauri wa jinsi ya kumtibu mgonjwa aliye taabani. 
Hivi sasa hospitali nne nchini zimeunganishwa katika mradi  huo wa Telemedicine ambazo ni Mwananyamala, Amana, Temeke na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) pamoja na hospitali ya Tumbi, Mkoa wa Pwani.
Mei, 2011 ndiyo wakati ambao Rais Jakaya Kikwete alizindua  mradi huu akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa India, Dk Manmohan Singh.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Modou Gaye anasema teknolojia hii inawezesha madaktari walioko katika Hospitali za Amana, Mwananyamala, Temeke, Tumbi na Bagamoyo kuwasiliana moja kwa moja na madaktari bingwa pamoja na watalaamu wengine walioko Muhimbili katika kujadili, kushauriana na hatimaye kufanya uamuzi kuhusiana na tiba, uchunguzi wa mgonjwa husika.
Gaye anasema kuwa teknolojia hii itamwezesha mgonjwa aliyeko kati ya hospitali hizo kupata matibabu bila kufika Muhimbili.
Anasema kupitia teknolojia hii wataalamu wataweza kuwasiliana katika nyanja za ushauri, vipimo vya uchunguzi mathalan vya radiolojia,  vipimo vya uchunguzi vya patholojia, magonjwa ya moyo na mafunzo kwa watalaamu.
Uwepo wa teknolojia hii utawezesha mgonjwa anayehitaji kupata huduma za kibingwa Muhimbili kutibiwa haraka na kwa muda mfupi kuliko ambayo angefuata utaratibu wa rufaa na hivyo kumpunguzia muda wa kukaa hospitalini kwa muda mrefu.

>>>MWANANCHI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright NTEL TANZANIA
Back To Top